Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, May 12, 2017

Upinzani nchini DRC wasema mwili wa mwanasiasa Etienne Tshisekedi hautarejeshwa nyumbani wiki hiii

media
Mwili wa kiongozi wa upinzani nchini DRC Etienne Tshisekedi
Chama kikuu cha Upinzani cha UDPS nchini  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kimeahirisha mpango wa kuurejesha nyumbani mwili wa aliyekuwa kinara wa chama hicho Etienne Tshisekedi.
Awali, mpango wa kuurejesha nyumbani mwili wa Tshisekedi ulipangwa kufanyika Mei 12.
Katibu mkuu wa chama hicho Jean-Marc Kabund, ameiambia RFI kuwa wameamua kuahirisha mpango huu, ili wapate muda wa kujadiliana na wakuu wa serikali kuhusu taratibu za kutoka jijini Brussels.
Kabund ameongeza kuwa hali ya wasiwasi imeenea katika maeneo jirani na ofisi za chama hicho jijini Kinshasa, ambapo mazingira yaliyopo si ya kuridhisha kutokana na idadi kubwa ya maafisa wa Polisi wanaonekana wakipiga kambi.
Msemaji wa vyama vya kisiasa vinavyomuunga mkono rais Joseph Kabila, Alain Atundu amesema serikali inafuatilia kwa karibu mpango huo, na imejipanga kuhakikisha mazishi ya kinara huyo wa upinzani yanafanyika kwa heshima.
"Viongozi wakuu wa serikali wanafanya kila jitihada kuhakikisha mazishi hayo yanafanyika katika hali yab heshima kulingana na kanuni pia sheria za nchi tangu mwaka 1914 kuhusu maeneo ya kuzika watu, hairuhusiwi kuzika mfu ndani ya mita hamsini na eneo lenye makazi ya watu," alisema Atundu.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa chama cha UDPS Rubens Mikindo amesema kuahirishwa kwa mpango huo inatoa nafasi ya mazungumzo kuhakikisha kuwa mazishi ya kinara huyo yanafanyika mwezi huu.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment