Dodoma. Serikali imesema itajenga daraja la juu kwa ajili ya kivuko cha waenda kwa miguu (Overhead pedestrian bridge) eneo la Kawe Bondeni.
Hayo yamesemwa bungeni leo (Jumatano) na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isack Kamwelwe aliyekuwa akijibu swali la Mbunge wa Kawe, Halima Mdee.
“Tatizo la kivuko cha waenda kwa miguu eneo la Kawe Bondeni hadi Jeshini Kata ya Mbezi Juu na Kawe, tayari limeshapatiwa ufumbuzi,” amesema.
Kamwelwe amesema kwa sasa mkandarasi wa kujenga daraja hilo yupo kwenye hatua za maandalizi ya kuanza ujenzi katika eneo hilo muhimu.
Pia amesema Serikali ina mpango wa kuweka taa za kuongozea magari katika barabara ya Mwenge-Tegeta na kwamba mkandarasi wa kuweka taa hizo ameshapatikana.
No comments
Post a Comment