Mgombea wa uwakilishi wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala) kwa upande wa Chadema, Salum Mwalimu ametumia jina la Rais John Magufuli, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe kujinadi.
Wakati akihitimisha maombi yake ya kura baada ya kuulizwa maswali matatu na wabunge, Mwalimu amesema atakapovuka mpaka wa Tanzania kuiwakilisha katika mataifa mengine kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki endapo atachaguliwa atakuwa mwakilishi wa Taifa na si chama.
Mwalimu amesema hata akivuka mpaka Rais ni (John) Magufuli, Waziri Mkuu ni(Kassim) Majaliwa na (Freeman) Mbowe atabaki kuwa mwenyekiti wa chama, hivyo kuwahimiza wabunge kumchagua bila kujali itikadi za chama.
Wagombea wengine wa nafasi hiyo kwa Chadema ni Profesa Abdallah Safari, Pamela Massay, Ezekia Wenje, Lawrence Masha na Josephine Lemoyan
No comments
Post a Comment