Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, May 10, 2017

Rais Putin , ajisifu hana mbabe duniani , azindua silaha mpya


Putin alisema hayo wakati wa maonesho ya kila mwaka ya majeshi ya taifa hilo kuadhimisha Siku ya Ushindi ambayo hutumiwa kukumbuka ushindi katika vita hivyo.

Kwa mara ya kwanza, maonesho hayo ya kijeshi yalishirikisha makombora ambayo yameundwa mahsusi kwa vita katika maeneo yenye baridi kali ya Arctic.

Urusi inajenga kambi mpya za kijeshi Arctic.



"Hakuna nguvu zozote zitakazoweza kuwashinda watu wetu," Bw Putin alisema, na kulaani uharibifu na maafa yaliyosababishwa na Ujerumani wakati wa vita hivyo.

Muungano wa Usovieti ulipoteza zaidi ya watu 20 milioni, zaidi kuliko taifa lolote lile wakati wa vita hivyo.

Muungano wa Usovieti (USSR) ulivunjika mwaka 1991.
Rais wa Ukraine Petro Poroshenko naye alishiriki katika sherehe ya kuweka shada la maua katika makumbusho mjini Kiev.

Aliwaambia wanajeshi wa Ukraine kwamba Urusi inajaribu kutumia maadhimisho ya ushindi huo "kutimiza mahitaji yake ya kikoloni na upanuzi."

"Kremlin bado inajaribu kuiamrisha Ukraine kama ilivyofanya ilipodhibiti maeneo manne ya vita Ukraine miaka ya 1940."



Urusi imekuwa ikishutumiwa na kudaiwa kudunisha mchango wa nchi nyingine katika vita vya kushinda utawala wa Nazi nchini Ujerumani.

Mataifa ya Magharibi yaliiwekea vikwazo Urusi baada yake kutwaa udhibiti wa eneo la Crimea mwaka 2014.

Urusi pia imekuwa ikituhumiwa kuunga mkono wapiganaji wanaopigania kujitenga kwa maeneo ya mashariki mwa Ukraine.
Urusi imekanusha tuhuma kwamba inasaidia waasi hao kijeshi, lakini imekiri kwamba Warusi wa "kujitolea" wanasaidia waasi.

Jeshi la vijana
Miongoni mwa zana za kivita ambazo zilioneshwa Red Square Jumanne, kulikuwa na makombora ya Pantsir-SA ya kujilinda sana ya kutumiwa maeneo ya Arctic.

Kulikuwa na makombora ya Yars RS-24 ambayo yanaweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine. Makombora hayo yanaweza kutumiwa kurusha silaha za nyuklia.
Makombora ya nyuklia ya Yars RS-24: Maonyesho hayo yamefufua kumbukumbu za maonyesho ya kijeshi ya Muungano wa Usovieti enzi za Vita Baridi

Wanachama wa jeshi mpya la "vijana wazalendo" ambalo linaitwa Yunarmiya, pia walishiriki maonesho hayo kwa mara ya kwanza.

Hafla kuu ilifanyika Moscow, lakini maonesho mengine yalifanyika katika miji mbalimbali Urusi. Miji mingi iliyoandaa maonesho ni ile iliyoathiriwa sana na vita hivyo vya 1941-1945 ambavyo Urusi huviita "Vita Vikuu vya Kizalendo".
Wanajeshi wa majini wa Urusi: Jeshi la Urusi limekuwa likijisifia kutokana na uwezo wake wa kupigana vita maeneo ya Arctic

"Ili kuushinda ugaidi, na misimamo mikali na itikadi mpya za Nazi, tunahitaji ushirikiano wa jamii yote duniani," Bw Putin alisema kwenye hotuba fupi.
Urusi imekuwa ikitumia silaha zake mpya katika vita vya Syria, ambapo wanajeshi wa nchi hiyo wanasaidia wanajeshi watiifu kwa Rais Bashar al-Assad.

Wanajeshi wa Assad pia husaidiwa pakubwa na Iran.

« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment