Writen by
sadataley
10:59 AM
-
0
Comments
Wosia ni jambo kati ya mambo ambayo huwasumbua watu wengi.
Sababu ya kuwasumbua wengi ni lile lile tu kuwa ufahamu wa mambo ya sheria haujawa wa kutosha katika jamii.
Tatizo la wosia limepelekea magomvi makubwa ya kifamlia hasa wakati wa misiba au baada ya misiba.
Pia wakati mwingine ni tatizo hili hili ambalo limewafanya baadhi ya watu tena ndugu kugombea maiti.
Kama watu wanaelewa vyema habari ya wosia na haki za kila mtu katika wosia sioni haja ya ndugu kugombea maiti au baadhi ya mambo ambayo marehemu pengine ameyatolea ufafanuzi kabla ya kifo chake.
Kuna wosia wa aina mbili,.
Leo sisi tunaangalia wa maneno
1. WOSIA NINNINI.
Tangazo la Serikali Nambari 436 la mwaka 1963 ambalo linajumuishasheria za kimila linatafsiri wosia kama, 'kauli inayotolewa na mtu wakati wa uhai wake kwa hiari yake kuonesha nia yake jinsi gani angependa mali yake igawanywe baada ya kufa kwake'.
Hilo ni tamko la serikali ni moja ya tafsiri ya maana ya wosia.
Pengine twaweza kusema tafsiri hii haijitoshelezi sana .
Tuna sema hivyo kwakuwa tafsiri hiyo haiingizi baadhi ya mambo ya msingi japo ni tafsiri halali.
Tafsiri nzuri zaidi inayoingiza mambo mengi ni hii,
Wosia ni tamko au maandishi anayotoa mtu wakati wa uhai wake akielezea mazishi yake yatakavyo fanyika akionyesha mahali atakapozikwa au jinsi mali zake zitakavyogawiwa kwa warithi wake baada ya kifo chake.
Kwa tafsiri hii ni kwamba wosia waweza kuwa maandishi au tamko.
Lakini pia wosia hauoneshi tu mgawanyo wa mali za marehemu isipokuwa unaonesha pia namna ya kufanya mazishi na mahali atakapozikwa mtu baada ya kifo chake.
2. WOSIA WA MANENO NININI.
Kwanza wosia huu wakati mwingine huitwa wosia mdomo, wosia maneno, au wosia wa tamko/matamshi.
Maana ya wosia huu ni kuwa ni tamko analotoa mtu wakati wa uhai wake akielezea mazishi yake yatakavyo fanyika likionyesha mahali atakapozikwa au jinsi mali zake zitakavyo gawiwa kwa warithi wake baada ya kifo chake.
Kwahiyo hili ni tamko tu basi.
Hapa hamna andishi lolote linalohusishwa ni mtu anaongea kama kuongea kulivyo.
3.WOSIA WA MDOMO LAZIMA USHUHUDIWE MASHAHIDI WASIPUNGUA WANNE.
Wosia huu unapaswa kushuhudiwa na mashahidi wasiopungua wa nne.
Ina maana ni kuanzia watu wanne kwenda mbele.
Mashahidi watatu, wawili, mmoja hawaruhusiwi .
Aidha mashahidi hao sio kwamba mtoa wosia anawachagua kwa namna anavyotaka kwakuwa usia ni wake.
Sheria imemwekea mipaka maalum mtoa wosia anayopaswa kuzingatia wakati wa kuteua mashahidi wake wa wosia.
Hatua hii ilizingatia matakwa ya msingi ya jamii zetu.
Sheria inataka mashahidi wawili kati ya mashahidi hao wawe ni wa ukoo wa huyo mwosia.
Hapa kuna mambo mawili kuna familia kuna na ukoo. Sheria inasema ukoo .
Ukoo ni mkubwa kuliko familia, ni zaidi ya fanilia .
Hivyo basi sheria inaposema mashahidi wawili watoke ndani ya ukoo mtu asilazimishe kwamba lazima watoke ndani ya familia..
Haya yapo ndio maana naweka msisitizo. Aidha wawili waliobaki wanaweza kutoka nje ya ukoo wa mwosia. Anaweza kuwa jirani, rafiki wa familia au mwingine yeyote mtoa wosia atakayemuona anafaa kushuhudia wosia wake.
4. KUBADILISHWA KWA WOSIA WA MDOMO.
Wakati wowote mtoa wosia akiamua anaweza kufuta wosia wa awali kwa ajili ya mabadiliko au vinginevyo.
Kama ni kufuta kwa ajili ya mabadiliko anaweza kuandaa mwingine kwa mdomo kama alivyofanya awali huku akibadilisha mashahidi au akitumia walewale au akabadilisha kutoka wosia wa mdomo kwenda wa maandishi kwa maudhui ile ile au kwa mabadiliko katika maudhui.
5. WARITHI HAWAWEZI KUWA MASHAHIDI.
Ni haramu kisheria mmoja wa watu ambao ni warirhi kuwa shahidi katika wosia.
Si tu haramu bali pia ni kihoja. Mchezaji hawezi tena kuwa refa
6. MAMBO MENGINE MUHIMU KATIKA WOSIA WA MANENO.
Kwanza mtoa wosia awe amefikisha umri wa miaka kumi na nane.
Awe na akili timamu wakati anatoa wosia huo, wosia ueleze bayana nani atausimamia, ueleze bayana nani ni warithi, pia zingatia sana wosia ni siri mpaka baada ya kifo cha muusiaji.
7. WOSIA WA MANENO NI KWA AJILI YA WASIOJUA KUSOMA NA KUANDIKA.
Izingatiwe kuwa wosia wa maneno ni kwa ajili ya watu wasio jua kusoma na kuandika.
Anayejua kusoma na kuandika basi na afanye wosia wake kwa maandishi. Aidha wosia wa maandishi utaelezwa vyema makala zijazo.

- Kwanza wa maandishi
- pili wa maneno.

No comments
Post a Comment