Writen by
sadataley
10:03 AM
-
0
Comments
Wananchi wa Gambia huko magharibi mwa Afrika wanatazamia kuelekea kwenye masanduku ya kupigia kura kwa ajili ya kuwachagua wawakilishi wao wa bunge baada ya kupita miaka 22.
Wananchi wa Gambia ambao hawakuwahi kushiriki kwenye uchaguzi huru unaovishirikisha vyama vingi wakati wa utawala wa Rais Yahya Jammeh aliyeshika hatamu za uongozi nchini humo kwa muda wa miaka 22, kesho Alhamisi watashiriki katika uchaguzi wa bunge kuwachagua wawakilishi wao katika chombo hicho cha kutunga sheria.
Usajili wa wagombea wa viti vya ubunge nchini Gambia ulimalizika jana Jumanne huku jumla ya wagombea 239 kutoka vyama tisa vya kisiasa wakiwa tayari kuchuana katika uchaguzi huo wa bunge. Katiba ya Gambia inasema kuwa, Rais ana mamlaka ya kuteuwa wabunge watano tu wa viti maalumu kati ya wabunge 53 wa bunge la nchi hiyo. Kabla ya hapo, Rais alikuwa na mamlaka ya kuwateuwa wabunge wa viti maalumu 43.
Chanzo ni parsday.com
No comments
Post a Comment