Writen by
sadataley
8:05 AM
-
0
Comments
Mwamuzi huyo wa pembeni alikumbana na kipigo hicho wakati wa pambano kati ya Nyota dhidi ya Bodaboda lililopigwa kwenye Uwanja wa Shuile ya Msingi
Mringa zikiwa zimesalia dakika 10 huku matokeo yakiwa bao 1-1.
Mashabiki hao wa Nyota walimvamia mwamuzi huo kwa kumuonyesha kibendera straika wao wakati akielekea kufunga na kuamini timu yao inanyongwa mbele ya wapinzani wao wanatokea Karatu.
Kufuatia kitendo hicho Frat Arusha wameonyeshwa kukerwa na Mwenyekiti wao, Soud Abdi, alisema hakuna haki inayopatikana kwa kuchukua sheria mkononi na kudai kitendo hicho ni ukiukwaji wa kanuni na sheria za soka na hata za nchi.
“Tunalaani kitendo hiki na tunatoa onyo kwa wahusika wote yaani klabu zijipime na wajirekebishe, maana hakuna anayejua sheria na kanuni na taratibu za soka zaidi ya mwamuzi na kama anakosea hakuna sheria ya kumpiga bali zifuatwe taratibu za malalamiko yanayoweza kushughulikiwa sio sheria mkononi.”
Mwamuzi huyo alijeruhiwa vibaya katika tukio hilo kiasi kwa kuwahishwa hospitali ya Mkoa Mount Meru ili kupatiwa matibabu ambayo ilibainika kaumia mbavu na maeneo mengine ya mwili wake
No comments
Post a Comment