Writen by
sadataley
11:35 AM
-
0
Comments
Naibu mshauri wa maswala ya usalama wa rais wa Marekani Donald Trump
ameombwa na serikali hiyo ajiuzulu baada ya miezi mitatu pekee ya uteuzi
wake kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.
Hatua hiyo inajiri baada ya Trump kumuondoa afisa wa mipango Steve Bannon katika baraza la usalama la taifa hilo.
Baraza hilo humshauri rais kuhusu maswala ya usalama wa kitaifa pamoja na maswala ya kigeni.
Uteuzi wa Banon mwezi Januari ulizua hofu kwamba swala la washauri wakuu lilikuwa likiingiziwa siasa.
Wachanganuzi wanasema kuwa hatua hiyo ya hivi karibuni inaonyesha kuwa mshauri mpya wa rais Trump kuhusu maswala ya usalama Luteni Jenerali McMaster analifanyia mabadiliko baraza hilo la NSC liliteuliwa na mtangulizi wake.
Aliyekuwa mshauri wa maswala ya usalama Luteni Jenerali Michael Flynn alifutwa kazi baada ya wiki tatu na siku tatu pekee, baada ya kubainika alimdanganya makamu wa rais kuhusu mazungumzo yake na balozi wa Urusi nchini Marekani.
No comments
Post a Comment