Chama cha Mawakala na Makarani wa Usafiri wa Abiria jijini Dar es Salaam umesema hautambui mgomo wa wamiliki wa vyombo vya usafiri uliotangazwa na Chama cha Wamiliki wa Mabasi nchini TABOA uliopangwa kufanyika keshokutwa Jumanne.
Chama hicho kimepinga mgomo huo kwa maelezo kuwa mgomo huo haukufuata misingi ya uendeshaji wa huduma za usafiri.
Akizungumza katika mahojiano na KURASA ya EATV katika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo hii leo; Mwenyekiti wa Mawakala na Makarani hao Bw. Khamisi Juma Iddi amesema kinachofanywa na wamiliki wa mabasi ni sawa na kuanzisha utawala ndani ya utawala pasipo kujali wadau wengine muhimu katika sekta ya usafirishaji.
Bw. Juma Iddi amesema wao kama mawakala na makarani wataendeleo kutoa huduma kama kawaida huku akiisihi serikali kuwa makini na wamiliki wa vyombo vya usafirishaji abiria kutokana na kile alichodai kuwa ni mwenendo wao unaotia mashaka.
No comments
Post a Comment