Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, April 11, 2017

Mahakama ya marekani yaiomba Tanzania kumsafirisha ‘kigogo wa unga’ Shkuba


Mahakama ya  Texas marekani imeiomba serikali ya Tanzania kumsafirsha anayedaiwa kuwa ni kinara wa mtandao wa kusamba za Kusafirisha Dawa za Kulevya Afrika Mashariki Raia wa Tanzania Ali Khatib Haji Hassan maarufu ‘Shkuba’. Inaandikwa na Faki Sosi.

Maombi hayo yamesomwa leo  na wakili Kakolaki mbele ya Hakimu Mfawidhi Cyprian Mkeha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu waliyowasiliswa pamoja na viapo vya maofisa wa marekani
Katika kiapo hicho maofisa wa marekani wandai kuwa mtuhumiwa huyo pamoja na wenzake walisambaza dawa za kulevya aina ya Heroin zaidi ya kilomoja nchi marekani.
Watuhumiwa wengine ni pamoja na Idd Mfuru, Tika Emmanuel Adam.
Katika viapo hivyo vyenye picha za washtakiwa wote watatu viliiomba mahakama kuridhia kusafirshwa kwa watuhumiwa hao na kupeleka mbele ya Mahakama ya Texas Marekani ambapo tayari kesi zidi yao imeshafunguliwa na mahakama hiyo imetoa hati ya kukamatwa kwao.
Kesi hiyo inaendelea Mahakamani kisutu mtandao huu utakujuza maamuzi yatakayotolewa
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment