Writen by
sadataley
9:46 AM
-
0
Comments
Jumuiya ya kimataifa imelaani shambulio linaloshukiwa kuwa la gesi ya kemikali dhidi ya mji unaodhibitiwa na waasi nchini Syria, shambulio linaloripotiwa kuua watu takriban 58.
Shirika la kimataifa linalopambana na matumizi ya silaha za kemikali OPCW limesema linakusanya ushahidi.
Naye mkuu wa sera za mambo ya nje ndani ya Umoja wa Ulaya, Federica Mogherini amesema pande zote na wadau kwenye vita ya Syria wanatakiwa kupata suluhu ya kisiasa
Akizungumza na wanahabari baada ya mkutano kuhusu mustakabali wa Syria, Mogherini amesema EU inategemea kila mmoja kutimiza wajibu wake kumaliza vitendo vya umwagaji damu.
''sisi Umoja wa Ulaya, si tunaotekeleza mashambulizi, sisi si tunaopigana, sisi ndio tunaotoa misaada ya kibinaadam, kuusaidia Umoja wa mataifa kufikia makubaliano na suluhu ya kisiasa na sisi ndio tunaokuwa tayari kuwasaidia raia wa Syria kujenga mustakabali wao kwa ajili ya taifa lao, hii ndio njia tunayotumia, hii ndio namna tunavyoamini sera ya nje inavyopaswa kutekelezwa, na tunasisitiza hilo, lakini haimaanishi kuwa mtu aharibu kila kitu kisha tulipe gharama. hili kamwe haliwezi kutokea'' alieleza
Kufuatia shambulio la anga jimboni Idlib kulitolewa ripoti zikisema kuwa mamia ya watu hasa watoto walikuwa wakitapika, kupaliwa na kutoja povu mdomoni
Serikali ya Marekani imesema shambulio lililotekelezwa Syria ni la kukemewa. Msemaji wa Serikali Sean Spicer ameinyooshea kidole serikali ya Rais wa Syria, Bashar Al Assad kuhusika na mashambulizi hayo.
Syria imekana kutumia silaha za kemikali.Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa litakutana kwa dharura siku ya Jumatano kujadili shambulizi hilo.
BBC Swahili
No comments
Post a Comment