HUDUMA za Usafiri zinaendelea kama kawaida kwenye kituo cha Mabasi cha Ubungo. Muungwana Blog imefika katika kituo hicho cha mabasi yaendayo mikoani asubuhi hii na kukuta huduma zikiendelea kama kawaida.
Hatua hiyo imefikiwa Siku moja baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri na Nchi Kavu na Majini, Sumatra, pamoja na wadau wa sekta ya usafirishaji kukubaliana kusitisha mgomo wa usafirishaji wa abiria na mizigo uliopangwa kuanza leo.
Akizungumza jan jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Gilliard Ngewe amesema kusitishwa huko kunatokana na kikao na Waziri wa Mawasiliano Uchukuzi na Ujenzi, Prof. Makame Mbarawa, kuhusu kuandika kwa kutenganisha makosa ya dereva na wamiliki wa mabasi
Bw. Ngewe alisema, kanuni hizo zitaandikwa ndani ya siku 14 katika rasimu hiyo na wadau wa usafirishaji kuendelea na shughuli za usafirishaji na kwamba, baada ya kufanya marekebisho ya rasimu ya kanuni itarudishwa kwa wadau kuweza kujadiliwa kwa ajili ya kuwasilishwa Bungeni .
Naye Makamu Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mabasi, Taboa, Abdallah Mohamed, alisema wamekubaliana na Sumatra kurekebishwa kwa baadhi ya kanuni za makosa kati ya wamiliki na madereva wa mabasi.
No comments
Post a Comment