Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, February 3, 2017

MBUNGE MCH PETER MSIGWA KUTOA MOTISHA YA TSH MILIONI 1.5 KWA LIPULI FC KESHO AWATAKA WABUNGE WENGINE KUISAIDIA LIPULI FC

Wakati kesho jumamosi timu ya wanaIringa Lipuli Fc inaingia katika mchezo wake muhimu wa kuingia kucheza ligi kuu ya VPL baada ya kuwa na uhakika wa kutwaa pointi 3 zilizosalia,  wadau  wa mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa
( Chadema) wameahidi kutoa motisha ya Tsh milioni 1.5 kwa timu ya Lipuli Fc .

Katika taarifa iliyotolewa na Mbunge Msigwa ambae yupo mjini Dodoma kuendelea na vikao vya bunge amesema yupo tayari kesho kuungana na wabunge wengine wa mkoa wa Iringa kuja kuishangilia timu ya Lipuli fc pamoja na mashabiki wengine.

Uzalendo huu ambao mbunge wetu aendelea kuonyesha ni wazi ligi kuu Iringa ipo mbioni kufanyika mkoani hapa  msimu ujao.

Tayari wabunge mbali mbali kama Ritta Kabati , Venance Mwamoto ,Costa Chumi, Mahamudu Mgimwa, Godfrey Mgimwa na wengine wameendelea kuisaidia timu ya Lipuli Fc .

Iwapo upo tayari kuchangia Lipuli Fc Tuma mchango wako kuanzia tshs 10,000/= kwenda namba 0713446699  na 0754695874  *zote Abousufian Silia...
Habari wa hisani ya Mtanda wa Matukio daima

« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment