WASANII wa Bongo wameitikia wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda wa kufika katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam mapema leo asubuhi.
RC Makonda jana aliwataja wasanii 9 wanaotuhumiwa kujihusisha na mtandao wa madawa ya kulevya pamoja na baadhi ya askari polisi huku akiwataka wafike kwenye Kituo Kikuu cha Polisi leo asubuhi kwa ajili ya mahojiano.
Mwingine ambaye mpaka sasa ameshawasili ni Mmiliki wa Klabu ya Usiku ya Element aliyewasili majira ya saa 5.00 akiambatana na mawakili wake wawili.
T.I.D naye akiwasili kituoni hapo saa 5:07 asubuhi.
Hamidu Chambuso aka ‘Nyandu Toz’ akiwasili kituoni majira ya saa 5: 38.
Babuu wa Kitaa akiwasili Kituo Kikuu cha Polisi majira ya saa 4: 38
Wanahabari wakichukua matukio kituoni hapo.
No comments
Post a Comment