Rais wa Marekani Donald Trump ametia saini agizo linaloidhinisha kuanza kujengwa ukuta katika mpaka wa Marekani na Mexico.
Agizo hilo ni mojawapo ya ahadi za Rais Trump wakati wa kampeni ambapo aliazimia kujenga ukuta wa zaidi ya kilomita 3,000 kuitenganisha Marekani na Mexico kwa lengo la kudhibiti wahamiaji kutoka Mexico kwa madai kuwa wanachangia kuleta matatizo mengi nchini Marekani yakiwemo ya dawa za kulevya, uhalifu na ubakaji.
Amesisitiza kuwa gharama ya ujenzi wa ukuta huo italipwa na Mexico, suala ambalo hata hivyo Rais wa Mexico imelipinga vikali na kuapa kutolipa fedha yeyote.
Bunge la Marekani litahitaji kuidhinisha agizo hilo la Rais Trump kabla ya utekelezaji. Wakati huo huo Rais Trump alitarajiwakukutana na Rais wa Mexico ikulu ya ya Marekani mwishoni mwa mwezi huu.
No comments
Post a Comment