Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, January 26, 2017

Paul Makonda ametangaza mfumo mpya kwa madereva Taxi jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametangaza mfumo mpya kwa madereva Taxi jijini Dar es Salaam ambao unatarajiwa kuanza hivi karibuni ukihusisha matumizi ya mashine maalum ya kutoa risiti kwa abiria na nauli kutozwa kutokana na umbali tofauti na makadirio yanayofanyika sasa.

Lengo la mfumo huo ni kuboresha mapato ya serikali, kuhakikisha abiria analipa nauli iliyosahihi pamoja na kuimarisha usalama wa abiria kufuatia kubainika kwa Vitendo vya wizi na Uporaji vinavyofanywa na baadhi ya madereva wa taxi hususan zisizosajiliwa.

Akizungumza katika Mkutano wa pamoja na madereva wa taxi katika jiji la dsm, maafisa wa mamlaka ya mapato tanzania TRA, kamanda wa kamati ya ulinzi ya mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema utaratibu uliopo sasa umepitwa na wakati kutokana na abiria kutozwa fedha nyingi bila kuzingatia Umbali, pamoja na kutokuwepo kwa usalama wa kutosha kwa abiria kutokana ongezeko la taxi bubu.

Kwa upande wao viongozi wa madereva hao wamedai kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo utitiri wa taxi bubu, kutozwa kiasi kikubwa cha kodi na ada mbalimbali , kuzagaa kwa bajaji katikati jiji .
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment