Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, December 6, 2016

Maelfu waomboleza kifo cha 'Iron Lady' wa India Jayalalithaa Jayaram

Jayalalitha

Image copyright@AIADMK
Image captionMwili wa Jayalalitha ukiwa umevikwa bendera ya India
Maelfu ya waombolezaji wamejitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa Jayalalithaa Jayaram, mmoja wa wanasiasa mashuhuri nchini India,.
Mkuu huyo wa serikali ya jimbo la Tamil Nadu alipatwa na mshtuko wa moyo Jumapili usiku na akafariki saa 23:30 (18:00 GMT) siku ya Jumatatu, kwa mujibu wa hospitali ya Apollo, mjini Chennai.
Mwili wake, ukiwa umevikwa bendera ya India, umewekwa kwa ajali ya kutazamwa na umma katika ukumbi mkubwa katika makao makuu ya jimbo hilo.
Polisi wa ziada wametumwa kudhibiti waombolezaji na kushika doria huku kukiwa na wasiwasi wa kuzuka kwa fujo.
Alikuwa anaenziwa sana na wafuasi wake, baadhi ambao walikuwa wanamwita "Amma" (mama) na kuna wasiwasi kwamba huenda baadhi wakaamua kujidhuru au kuzua ghasia.
Awali, baada ya taarifa za kifo chake kutangazwa, kulitokea makabiliano kati ya polisi na wafuasi wake nje ya hospitali hiyo ya kibinafsi ya Apollo. Taarifa hizo baadaye ziliondolewa, ingawa saa chache baadaye alithibitishwa kufariki.
Baadhi ya wafuasi wake wamekuwa wakilia hadharani na kujipiga vichwa na vifuani.
Maelfu ya watu wamejitokeza kutoa heshima zao za mwishoImage copyright@AIADMK
Image captionMaelfu ya watu wamejitokeza kutoa heshima zao za mwisho
Jimbo la Tamil Nadu limetangaza siku saba za maombolezi.
Serikali kuu mjini Delhi nayo imetangaza Jumanne kuwa siku ya mapumziko ya kitaifa kama heshima kwake.
Waziri Mkuu Narendra Modi atahudhuria ibada ya mazishi ya kiongozi huyo ambayo yatafanyika baadaye Jumanne.
Jayalalithaa JayaramImage copyrightAFP
Image captionKumekuwa na wasiwasi kwamba huenda wafuasi wake wakazua fujo
ChennaiImage copyrightAP
Image captionBaadhi walikimbiza gari la kubeba wagonjwa lililobeba mwili wake
ChennaiImage copyrightAFP
Image captionTaarifa za kupotosha kuhusu kifo chake awali ziliwafanya wafuasi wake kulia kwa huzuni
Supporters hold a photograph of Tamil Nadu state leader Jayalalithaa JayaramImage copyrightAFP
Image captionWafuasi wa Jayalalitha wakiwa na picha yake
Maafisa zaidi wa polisi wametumwa ChennaiImage copyrightAP
Image captionMaafisa zaidi wa polisi wametumwa Chennai
A supporter of Tamil Nadu Chief Minister Jayalalitha Jayaraman holds her photo at the AIADMK party office in Mumbai, India, December 5Image copyrightREUTERS
Image captionMsako wa polisi miaka ya 1990 uligundua sari 10,500 na jozi 750 za viatu nyumbani kwa Jayalalitha
Jayalalitha aliishi maisha yenye visa vingi, hadharani na faraghani.
Aliigiza katika zaidi ya filamu 100 kabla ya kujiingiza katika siasa.
Jayalalitha baadaye alichukua udhibiti wa chama cha AIADMK kutoka kwa mke wa mwanzilishi wa chama hicho, na kisha akashinda uchaguzi 1991.
Alikuwa ametuhumiwa kwa kujihusisha na ufisadi, na alikaa jela vipindi viwili vifupi, karibuni zaidi 2014.
Mahakama kuu mjini Karnataka ilimuondolea makosa mwaka 2015 na akarejea uongozini.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment