Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, December 1, 2016

Gambia kufanya uchaguzi leo

Gambia

Image captionRais wa Gambia Yahya Jammeh
Wapiga kura nchin Gambia wanajiandaa kwenda katika vituo vya kupigia kura tayari kumchagua Rais Afrika Magharibi nchini Gambia .
Yahya Jammeh ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1994 atachuana na muungano wa vyama vya upinzani.
Inaarifiwa kuwa vyama saba vimeamua kuunganisha nguvu zao na kumpa kibali mgombea mmoja Adama Barrow ambaye anatafsiriwa kama tishio kwa Rais Yahya Jammeh.
Adama anatafsiriwa na watu wake wa karibu kuwa ni shababi ambaye aliweka rehani kwa wakala wa mali isiyohamishika miezi sita tu iliyopita ili kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho.
Pamoja na hayo yote rais Jammeh amejinasibu kuwa hatishwi na jambo lolote katika uchaguzi huo wakati huo huo wapinzani wake wanadai tabia zisizofaa zimemuandama rais huyo miezi kadhaa iliyopita kabla ya kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho.
Upande wa upinzani umekuwa ukipiga kampeni kwa nguvu zao zote katika siku za hivi karibuni, ingawa mpaka sasa viongozi wakuu wa vyama vya upinzani wako magerezani baada ya kufanya maandamano katika mitaa mbali mbali ya jiji la Gambia mnamo mwezi wa nne mwaka huu.
Mpaka sasa inaarifiwa kuwa serikali ya Gambia imekata mawasiliano yote ya simu ikiwemo mitandao huku wapinzani wakichelea mchezo mchafu kufanywa ikiwemo uvunjifu wa amani kwa hatua hiyo ya serikali.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment