Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, February 23, 2016

UN yashtumu matukio Uganda

Kuimeibuka taharuki kufuatia mauji ya watu wawili na vilevile kamata kamata ya kiongozi wa upinzani daktari Kizza Besigye Umoja wa Mataifa umeelezea hofu kuhusu hali ya taharuki iliyotanda nchini Uganda hususan baada ya uchaguzi mkuu wa urais uliokamilika majuzi Afisi ya haki za kibinadamu ya Umoja huo inaelezea wasiwasi kufuatia kuwepo kwa hali ya uhasama mkubwa baina ya rais wa jamhuri Yoweri Museveni na viongozi wa upinzani akiwemo kanali mstaafu Kizza Besigye. Kuimeibuka taharuki kufuatia mauaji ya watu wawili na vilevile kamata kamata ya kiongozi wa upinzani daktari Kizza Besigye kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya urais. Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda Dakta Besigye amepinga matokeo ya uchaguzi akisema kuwa haukuwa wa haki na huru. Umoja wa mataifa unaelezea jinsi maafisa wa usalama wamekuwa wakitumia nguvu kupita kiasi Katika taarifa yake Umoja wa mataifa unaelezea jinsi maafisa wa usalama wamekuwa wakitumia nguvu kupita kiasi wanapokabiliana na watu wasiokuwa na silaha ambao msimamo wao unaelekea upande wa chama cha upinzani FDC. ''Inatisha sana ukitizama shime ambayo polisi na jeshi la Uganda ilikuwa nayo ilipovamia afisi za chama cha FDC siku ya ijumaa '' taarifa hiyo inaelezea. Kerry amlalamikia Museveni kuhusu uchaguzi Dakta Besigye amepinga matokeo ya uchaguzi akisema kuwa haukuwa wa haki na huru. Juma lililopita waziri wa maswala ya kigeni wa Marekani John Kerry alizungumza na rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa simu na kumwelezea wasiwasi wake kuhusiana na matumizi ya nguvu kupita kiasi wanaposhughulika na wafuasi wa upinzani. Aidha Kerry alizungumzia swala la uhuru wa viongozi wa upinzani mbali na kujadili hatua ya serikali kufunga mitandao ya kijamii siku ya uchaguzi.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment