Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, February 22, 2016

Obasanjo: Uganda haipaswi kuzuia upinzani

Aliyekuwa rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo, ametaka pande zote pinzani katika uchaguzi wa Uganda kujiepusha na matamshi ya uhasama. Obasanjo ambaye aliongoza ujumbe wa Jumuiya ya madola uliokuwa ukiangalia vigezo vya kidemokrasia katika uchaguzi uliokamilika nchini Uganda amewashauri viongozi wa uganda kujiepusha na makabiliano na migongano baina yao. Obasanjo alisema''Uhuru wa kujieleza kutengamana na kuwasilana na umma wa kila kiongozi sharti ulindwe na kama kuna vizuizi dhidi ya kiongozi yeyote lazima iondolewe mara moja'' Uganda haifai kuwazuia viongozi wa upinzani ,Obasanjo aliyasema hayo bila ya kumtaja kiongozi wa upinzani Kizza Bisigye ambaye kwa sasa amezuiliwa nyumbani kwake. Aliongezea kuwa ''dosari zilizoshuhudiwa katika uchanguzi mkuu umekuwa na madhara mabaya kwa matokeo ya ukweli haki na uwazi wa uchaguzi huo'' , lakini amesisitiza tofauti kati ya utawala na upinzani zinahitajika kusuluhiswa kupitia mazugumzo.'' Kauli hiyo ya Obasanjo inawadia saa chache baada ya Kizza Besigye kukamatwa na polisi wa Uganda. Mtazamo wa Besigye kuhusu uchaguzi Kiongozi huyo wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda alikamatwa alipokuwa akijaribu kuondoka nyumbani kwake. Kiongozi huyo wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda alikamatwa Amekuwa kwenye kizuizi cha nyumbani tangu Ijumaa wakati polisi walimtuhumu kupanga kujitangazia matokeo. Wakili wake amethibitisha habari za kukamatwa kwake. Awali kulikuwa na habari kwamba angefika makao makuu ya Tume ya Uchaguzi kuitisha matokeo rasmi ya kina ya uchaguzi wa urais. Chanzo:BBC SWAHILI
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment