Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, July 1, 2015

Kivumbi wagombea urais 42 wa CCM

Dar. Hiki ni kivumbi. Kati ya wagombea 42 waliojitokeza kuwania urais kupitia CCM, anatakiwa kubaki mmoja tu na mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu unafungwa kesho. Kuimarisha uchumi kwa kutumia mbinu mbalimbali, kupambana na rushwa na ufisadi, kuboresha elimu, kukuza ajira kwa vijana na kuboresha uwajibikaji ni baadhi ya ahadi zilizotawala na makada 42 waliochukua fomu. Hadi sasa ni kada mmoja tu, Hellen Elinawinga ametangaza kutoendelea na mchakato huo. Gazeti la Mwananchi linapitia ahadi hizo kwa kifupi. Samweli Sitta Waziri huyo wa Uchukuzi ameahidi kupambana na rushwa, kutenganisha uongozi na biashara na kila mara amekuwa akisisitiza kuwa: “Nitahakikisha inaandaliwa sheria maalumu ambayo itawalazimisha watu kuchagua kati ya biashara na uongozi.” Dk Titus Kamani Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ameahidi kupambana na changamoto za afya, ajira na uchumi. Jingine ni kuangalia makundi ya watu wenye ulemavu wa ngozi, wanawake na wastaafu.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment