Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, July 1, 2015

Kivumbi wagombea urais 42 wa CCM part 2

Profesa Sospeter Muhongo Mbunge wa Kuteuliwa na Rais ameahidi kukuza uchumi kwa kusimamia mafuta, gesi, umeme na elimu ili kuwakwamua wananchi katika lindi la umaskini. Pia kukuza uchumi wa nchi kwa asilimia 7.5 hadi asilimia 10 mpaka 15 kwa kipindi cha miaka mitano au 10. Edward Lowassa Mbunge wa Monduli amepania kuinua vijana katika ajira, kusimamia Muungano, kuinua elimu na uchumi wa nchi kupita rasilimali za ndani. Pia, kutatua migogoro ya ardhi ya wakulima na wafugaji. Katika michezo ameahidi, kuhakikisha Tanzania inafanya vizuri katika ramani ya dunia na kwamba ataweka mkazo zaidi katika mchezo wa riadha. Mwigulu Nchemba Naibu Waziri wa Fedha amejitosa kupambana na umaskini, kusimamia ulipaji kodi ili kulipa Taifa mafanikio ya kiuchumi. Pia, kupinga utitiri wa kodi bila huduma husika na muhimu kutolewa na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha na rasilimali za umma. Balozi Amina Salum Ameahidi kusimamia uchumi na maendeleo, kitu ambacho kitakuwa na jukumu la kutoa ushauri wa haraka kuhusu maeneo na aina ya uwekezaji unaohitajika. Pia ameahidi kuondoa kasoro za mfumo dume ambao unachangia kudumaza huduma za msingi kwa wanawake. Profesa Mark Mwandosya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) ataanzisha kilimo cha kisasa na kisayansi kinachozingatia sifa zote za kilimo cha kisasa kwa kuboresha pembejeo na miundombinu. Pia atapambana na rushwa kwa kuondoa vikwazo vinavyozuia mapapa wa rushwa wasishughulikiwe na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). Frederick Sumaye Ameahidi kukuza uchumi kwa kuweka msukumo katika kilimo, kuboresha mbegu, kutafuta masoko na kusimamia viwanda vya ndani. Pia ataunda mahakama maalumu ya kushughulikia rushwa, ufisadi, uhujumu uchumi na biashara ya dawa za kulevya. Mizengo Pinda
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment