Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, June 30, 2015

Ugiriki yaomba miaka 2 kukomboa uchumi

Ugiriki imeomba mwafaka wa miaka miwili wa kuiokomboa kiuchumi kutoka kwa jumuiya ya ulaya. Mapendekezo yake yanajumuisha kufanya marekebisho mengi yatakayiwezesha kulipa madeni makubwa inayodaiwa. Tangazo hilo limetolewa karibu dakika za mwisho. Mapema ugiriki ilikuwa imethibitisha kuwa itashindwa kulipa deni lake kufikia mwisho wa siku na wanahabari wanatilia shaka mapendekezo haya ya anthens. Chanzela wa Ujerumani Angela Merkel alinukuliwa akisema mapema kuwa hakutazamia matokeo haya. Awali Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras aliwaomba wapiga kura wakatae masharti ya wakopeshaji wa nchi hiyo wakati wa kura ya maoni hapo Jumapili. Bw Tsipras amesema kwa kupinga kubana matumizi, Ugiriki itaweza kushauriana zaidi na kupata suluhu la mozozo wa sasa wa kifedha. Siku ya mwisho kwa Ugiriki kugharamia madeni yake ni Jumanne wiki hii ambapo inatakiwa kulipa deni la Euro bilioni 1.6, kwa shirika la fedha duniani{IMF}.Viongozi wa Muungano wa Ulaya wameonya hatua ya kukataa kulipa madeni yake ni sawa na Ugiriki kujiondoa kutoka kanda inayotumia sarafu ya Euro. Hata hivyo Waziri Mkuu Tsipras amesema hataki nchi yake kuitema Euro.Mazungumzo kati ya Ugiriki na wakopeshaji wake yalivunjika wiki jana, hatua iliyosababisha benki za nchi hiyo kufungwa.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment