Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, July 1, 2015

Kivumbi Urais part 4

Luhaga Mpina Mbunge huyo wa Kisesa ameahidi kukuza uchumi kwa kuongeza misingi ya upatikanaji wa fedha. Kuongeza mapato ya nchi na kuyasimamia kwa manufaa ya nchi na wananchi kwa ujumla. Lazaro Nyalandu Waziri wa Maliasili na Utalii ameahidi kujenga uchumi imara utakaosaidia kupunguza ukali wa umaskini kwa wananchi na kuwawezesha wananchi mmojammoja kupata kipato kulingana na shughuli anazofanya. Dk Augustine Mahiga Balozi huyo mkongwe ameahidi kuongeza kipato cha kati cha wananchi, kukuza uchumi kwa kupambana na umaskini kwa kutoa msukumo katika kilimo, viwanda, uchukuzi na utalii. Dk Mwele Malecela Mtaalamu huyo wa masuala ya tiba ameahidi kuhakikisha huduma za afya zinapatikana kwa watu wote, kutoa elimu ya ufundi ili kuongeza ajira kwa vijana, msukumo mkubwa ukiwa kukuza uchumi. Elidephonce Bihole Ameahidi kuwapeleka Watanzania katika nchi ya ahadi, kuinua uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo. Dk Hassy Kitine Amepania kuirudisha Tanzania ya Mwalimu Julius Nyerere, kuwa na sera sahihi za maendeleo ya nchi, kuinua kilimo, viwanda, uchukuzi, afya, elimu na kuinua maisha ya kila mwananchi.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment