Writen by
sadataley
8:19 PM
-
0
Comments
Dk Asha-Rose Migiro
Waziri huyo wa Katiba na Sheria ameahidi kutekeleza Ilani ya CCM kuendelea kukuza uchumi utakaowafikia wananchi walio wengi zaidi.
Joseph Chagama
Ameahidi kupambana na tatizo la ajira kwa vijana. Kusimamia utekelezaji wa Sheria , uadilifu na elimu.
Balozi Ali Karume
Mwanadiplomasia huyo ameahidi kuwapo kwa uhuru bila kujali dini, itikadi za vyama, elimu wala vyeo, kupambana kukuza kilimo kwanza na elimu baadaye anasema ni ngumu kusoma kama una njaa.
Makongoro Nyerere
Mbunge wa Afrika Mashariki anasema vipaumbele vyake vitatokana na ilani ya CCM.
Maliki Malupu
Ataboresha elimu, kilimo kwa kuwa na mbegu bora kuongeza msukumo katika kilimo chenye tija na kumwezesha mkulima mdogo kujikimu.
Dk Ghalib Bilal
Makamu wa Rais atasimamia uwajibikaji katika sekta ya umma, kulinda haki za binadamu na kuongoza kwa misingi ya sheria. Pia, kusimamia matumizi mazuri ya rasilimali za Taifa na kuboresha usimamizi wa mapato.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments
Post a Comment