Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, July 1, 2015

kivumbi part 6

Amos Siyantemi Atadumisha amani, kurudisha mfumo wa mabalozi wa nyumba 10, kuwafilisi mali wote watakaokamatwa na rushwa. Dk John Magufuli Waziri wa Ujenzi ameahidi kutekeleza kwa nguvu zote ilani ya CCM. Jaji Augustino Ramadhani Ameahidi kuyaangalia mapendekezo ya wananchi yaliyoachwa kwenye Katiba Inayopendekezwa na kuyatafutia dawa mapema matatizo yakiwamo ya rushwa, ufisadi na tatizo la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi. Dk Mussa Kalokola Amesema atakomesha unyanyasaji wanaofanyiwa Watanzania na kurejesha mfumo utakaoleta mchangamko wa uchumi, ambao unadorora kwa kukosekana uongozi bora. Ritta Ngowi Atakuza uchumi, kujenga kituo cha kulea kuwahudumia wastaafu, walemavu na wasiojiweza. Monica Mbega Atatekeleza ilani ya CCM na kuendeleza mazuri yaliyofanywa na waliotangulia. Nicholas Mulenda Atahakikisha CCM inakuwa imara zaidi. Banda Sonoko Ameahidi kuvaa viatu vya Mwalimu Nyerere kwa kusimamia nchi kujiendesha kwa kodi za nchi na kufufua uchumi wa viwanda. Helen Elinawinga Atapambana na adhabu za vifo kwa viongozi. Dk Harrison Mwakyembe Atatekeleza ilani ya CCM, kupambana na rushwa kwa nguvu zote. Mathias Chikawe Ataendeleza mapambano dhidi ya ujinga, maradhi na umaskini na kupiga vita ufisadi. Antony Chalamila Ameguswa kuwatumikia wananchi.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment