Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, January 8, 2015

Polisi Ufaransa watoa picha za washukiwa

Picha za washukiwa waliotajwa na polisi wa Ufaransa 
 Polisi wa Ufaransa wametoa majina na picha ya washukiwa wawili waliohusika na shambulio katika ofisi za jarida la vibonzo nchini humo.
Polisi wamemtaja Said Kouachi na kaka yake Cherif wanaweza kuwa watu hatari na wenye silaha.
Cherif Kouachi aliwahi pia na kuhusika na kupeleka wapiganaji wenye msimamo mkali wa kidini nchini Iraq.
Vyombo vya Habari vya Ufaransa vimesema mtu wa tatu ambaye amegunduliwa pia kama ni mshukiwa Hamyd Mourad mwenye umri wa miaka 18 alijisalimisha polisi baada ya kuona jila lake katika mitandao ya kijamii.
Baadhi ya rafiki zake walisema katika mitandao hiyo kwamba alikuwa shule wakati shambulio hilo katika ofisi za jarida la vibonzo la Charlie Hebdo likitokea, ambako watu 12 waliuawa.
Uchunguzi mkali bado unaendelea kuwasaka watu hao wenye silaha.
Awali jarida hilo lilipandisha hasira kwa waislamu baada ya kuchapisha kibonzo walichodai kuwa ni Mtume Muhamad SAW.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment