Writen by
sadataley
1:24 PM
-
0
Comments

Emmanuel Mbasha (katikati) akisindikizwa na wadogo zake, Onesmo
(kushoto) na Patrick wakati wanatoka Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini
Dar es Salaam jana. Mbasha alisomewa maelezo ya awali ya kesi ya tuhuma
za kubaka. Picha na Salim Shao.
Na Hadija Jumanne, MwananchiDar es Salaam. Ushahidi wa kesi inayomkabili mwimbaji wa nyimbo
za injili, Emmanuel Mbasha utaanza kusikilizwa Agosti 22, mwaka huu
katika Mahakama ya Wilaya Ilala.
Mbasha, ambaye ni mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili nchini, Flora Mbasha, anakabiliwa na mashtaka mawili ya ubakaji.
Mahakama imepanga tarehe hiyo kuanza kusikiliza ushahidi na upande wa mashtaka utakuwa na mashahidi wanne.
Jana mshtakiwa huyo alisomewa maelezo ya awali na Mbasha alikana baadhi ya maelezo na kuyakubali mengine.
Akisoma maelezo hayo, wakili wa Serikali, Nassoro
Katuga alidai kuwa Mei 23 mwaka huu katika nyumba ya mshtakiwa iliyopo
Tabata Kimanga, mshtakiwa alimuingilia kimwili msichana wa miaka 17,
walipobaki wawili katika nyumba hiyo.
Wakili Katuga alidai siku hiyo ya tukio mshtakiwa
alifanikiwa kufanya mapenzi na binti huyo na kumwambia asimwambie mtu
wakati mkewe akiwa hayupo nyumbani hapo.
Aliendelea kudai kuwa Mei 25, mshtakiwa alimwambia
binti huyo amsindikize kwenda kumtafuta Flora sehemu alipo na wakati
wanarudi kutoka huko, mshtakiwa alifanya mapenzi na binti huyo ndani ya
gari lake alilokuwa akiendesha mshtakiwa.
Katuga alidai Mei 26, mwaka huu, binti huyo alitoa
taarifa Kituo cha Polisi cha Osterbay akapewa PF3 na kwenda Hospitali
ya Amana kutibiwa na vipimo vya daktari vilithibitisha kuingiliwa
kimwili.
Wakili Katuga alidai baada ya binti huyo kutoa
taarifa polisi, Mbasha alitoweka nyumbani hadi Juni 16, mwaka huu,
alipofikishwa polisi na Juni 17 alipandishwa mahakamani hapo kujibu
mashtaka mawili ya kubaka.
No comments
Post a Comment