Writen by
sadataley
6:03 PM
-
0
Comments
Siku hiyo ya jumapili ya tarehe 6 Julai kwaya ya Uinjilisti Sayuni
kutoka usharika wa Kilutheri Kinondoni inatarajiwa kuweka wakfu DVD yake
ya tatu iitwayo 'Dua na Maombezi' katika ibada mbili zitakazofanyika
kanisani kwao Kinondoni na kufuatiwa na tamasha la uimbaji majira ya
mchana mara baada ya kuisha kwa ibada ya pili, ikisindikizwa na Beatrice
Moses, Amkeni, Fellowship Kinondoni pamoja na wana wa Gusa AIC
Chang'ombe.
Kwaya hiyo ambayo moja ya sifa zake ni kuimba live na kwaustadi zaidi
wakiimba kwa kumtukuza Mungu, wamekuwa katika mazoezi ya kuhakikisha
siku ya jumapili wanaimba kwa viwango zaidi lakini kubwa zaidi ni kuona
watu watakaofika wanakutana na uwepo wa Mungu katika uzinduzi huo ambao
makamu wa Askofu wa Dayosisi ya mashariki na pwani kanisa la Kilutheri
George Fupe pamoja na mkewe wanatrajiwa kuungana na kwaya hiyo katika
tendo hilo.
Kwaya ya Sayuni inafahamika vyema kwahuduma yake kwa wanafunzi wa Ukwata
kwa miaka mingi, lakini pia ndio kwaya ya kwanza kutoa album za
mapambio ambazo zilitokea kupendwa zikiwemo Yawe Yawe au Bwana wa
mabwana, parapanda italia, Simba wa Yuda, Bwana Yesu anakuja, Safari na
nyimbo nyinginezo. Mwenyekiti wa kwaya hiyo bwana James Makatta
amewataka wapenzi wa muziki wa injili kutokosa siku ya jumapili kwakuwa
itakuwa siku ya kukumbukwa kwa watakaohudhuria.
Aidha tukio lingine siku ya jumapili ni kwaya ya Neema Gospel kutoka
kanisa la AIC(T) pastorate ya Chang'ombe jijini Dar es salaam ambao
wamekuwa gumzo siku za karibuni kutokana na mabadiliko ya uimbaji wao,
wanatarajia kuachia album yao iitwayo 'Haki yake Mungu' ambayo imebeba
nyimbo nyingine ambazo zimetokea kupendwa sana kila wanapokwenda kwenye
mwaliko hususani kwenye ibada za kusifu na kuabudu katika kanisa la Dar
es salaam Pentecoste Kinondoni (DPC).
Kwaya hiyo ambayo ni kongwe imetokea kupendwa toka enzi hizo walipotoa
video yao ya kwanza 'Dunia imeoza' ikiwa na nyimbo mablimbali kama
sinyinyi mlionichagua ulioimbwa na solo matata wa kwaya hiyo mwanadada
Tabitha lakini kama haitoshi kwaya hiyo pia ambayo ndiyo aliyokuwa
akiimbia marehemu Steven Kanumba kabla hajaanza kuigiza walitoa video ya
pili inayoitwa 'Pengine Hukujua' na kufuatiwa na vieo ya tatu
inayopendwa mpaka leo iitwayo 'Kuna mamba kivukoni'.
Neema Gospel Choir wanatarajiwa kusindikizwa na waimbaji kama AIC Dar es
salaam Choir kutoka Magomeni, John Lisu na timu yake pamoja na kwaya
maarufu kutoka hapo hapo kanisani chang'ombe iitwayo AIC Chang'ombe wana
wa Gusa ambao pia wameahidi kufika katika uzinduzi wa kwaya ya Sayuni
Kinondoni siku hiyo ya jumapili. Matukio yote mawili hayatakuwa na
kiingilio chochote bali ni bure.
Habari na Gospel Kitaa


No comments
Post a Comment