Writen by
sadataley
3:27 PM
-
0
Comments
Na Mwandishi WetuSao Paulo, Brazil. Timu ya soka ya Argentina imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Dunia baada kuitungua Uholanzi kwa mikwaju ya penalti 4-2, katika mchezo wa jana wa nusu fainali nchini Brazil.
Kipa wa Argentina, Romero, alikuwa shujaa katika
mchezo huo baada ya kupangua penalti mbili na kuisaidia timu yake
kutinga katika hatua ya fainali, mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa
Corinthians mjini Sao Paulo.
Kwa matokeo hayo, Argentina sasa itavaana na
Ujerumani katika mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia nchini Brazil
jumapili katika Uwanja wa Maracana.
Uholanzi ilikuwa na mchezo wa kawaida tofauti na
ilipocheza na Costa Rica katika hatua ya robo fainali, huku kasi ya
Argentina ikionekana kubadilika kuliko ilivyokuwa katyika mchezo wao
uliopita.
Nafasi chache katika mchezo huo zilishindwa
kutumiwa vizuri na Arjen Robben, ambaye angeweza kuipa bao timu yakew
dakika ya 90, lakini kiungo Javier Mascherano alimuwahi kabla ya kuleta
madhara.
Mikwaju ya penalti iliyopigwa na Lionel Messi,
Sergio Aguero, Ezequiel Garay na Maxi Rodriguez zilitosha kuipa ushindi
Argentina huku Wesley Sneijder na Ron Vlaar wakikosa kwa upande wa
Uholanzi.
No comments
Post a Comment