Writen by
sadataley
3:29 PM
-
0
Comments
Na Oliver Albert, MwananchiDar es Salaam. Kocha wa JKT Ruvu, Fred Felix Minziro amesema katika maisha yake ya ukocha hatasahau kipigo cha mabao 5-0 walichokipata Yanga kutoka kwa Simba, msimu wa 2011/2012.
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano
maalumu jana, Minziro alisema: “Nilifungwa mabao 5-0 na Simba nikiwa
nimebaki kocha peke yangu katika benchi maana kocha mkuu Kostadin Papic
aligoma na kukaa jukwaani.
“Ilikuwa ni mechi iliyoshusha heshima ya klabu,
iliyotia simanzi na ambayo iliweka rekodi mbaya katika maisha yangu ya
ukocha, ndiyo maana mpaka sasa imebaki mawazoni mwangu, sitakuja
kuisahau,” alisisitiza.
Aliongeza: “Iliniuma sana siku ile kwani matokeo
yalipangwa, yaani mechi ile imebaki kwenye kumbukumbu yangu kwani hata
magoli yenyewe yaliyofungwa, yaani magoli yote yalipangwa siyo siri na
hakuna asiyefahamu hilo.
“Kipindi kile Yanga ilikuwa na mgogoro wa uongozi,
hivyo mechi ilipangwa tufungwe ili viongozi waonekane hawafai hasa
mwenyekiti wa wakati huo, Lloyd Nchunga na lengo lao wamwondoe,
lakini mimi nasema walimwonea kwani alikuwa ni kiongozi mzuri, ila ile
mechi sitakaa niisahau.”
Aliongeza :”Ukiangalia ile mechi jinsi wachezaji
walivyokuwa wanacheza unaona kabisa matokeo yalipangwa, wachezaji wangu
walicheza chini ya kiwango kuliko siku zote, unaona mabeki hawakabi,
viungo hawapambani, washambuliaji ndio kabisa hawakuonyesha kuwa
wanataka kufunga, yaani ilionyesha dhahiri kuna kitu kilipangwa. Sijui
kulikuwa na maelekezo, lakini sijui walipata wapi maelekezo hayo.”
Minziro alikuwa beki mahiri wa Yanga pia kocha
msaidizi wa klabu hiyo kabla ya Desemba mwaka jana kufukuzwa akiwa
pamoja na kocha mkuu, Mholanzi, Ernest Brandts.
Hata hivyo, Minziro aliwausia wachezaji waache
kutumika kama chambo kutoka kwa baadhi ya watu na kucheza chini ya
kiwango kwa maelekezo ya viongozi fulani kwani jambo hilo linashusha
heshima zao.
“Ninachowashauri wachezaji wacheze mpira hata
kama kuna mgogoro katika uongozi hawapaswi kuingilia hilo hata
wakiambiwa wacheze chini ya kiwango wao wanatakiwa kucheza kama siku
zote ili kutoharibu CV zao kwani ile mechi kuna wachezaji walijiharibia
kabisa mpaka sasa wamepotea katika ramani ya soka,” alisema.
No comments
Post a Comment