Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, July 12, 2014

ZAZA WA KIBAO CHA CALVARY AWASILI UINGEREZA, SPIRIT OF PRAISE KUREKODI MWEZI UJAO


Mwanamama Zanele (Zaza) akivinjari ndani ya jiji la London hapo jana.
Mwanamama Zanele Mokhethi almaarufu kama Zaza ambaye ni mwimbaji nyota wa muziki wa injili Afrika ya kusini, yupo jijini London nchini Uingereza kwa mwaliko wa kihuduma kupitia kanisa la Trinity Baptist ambalo lipo kusini mwa jiji la London mitaa ya Norwood.

Kwa mujibu wa Zaza ambaye ametokea kujizolea mashabiki mara baada ya kazi nzuri aliyoifanya kwenye Spirit of Praise toleo la nne, ameiambia GK kwamba amewasili siku ya jumanne wiki hii na
Ni mwendo wa matembezi kabla ya huduma.
kwamba anatarajia kufanya huduma katika makanisa mbalimbali likiwemo kanisa la Trinity Baptist siku ya jumamosi ijayo.
Zaza amezindua album yake mpya mapema mwezi ulioisha iitwayo 'Imvuselelo' huku pia akitarajiwa kuwasha moto kwa mara nyingine tena wakati kundi la Spirit of Praise litakapokuwa likirekodi dvd yake ya tano mapema mwezi ujao tarehe 2 August katika ukumbi wa Big Top Arena uliopo Carnival City nchini Afrika ya kusini huku tiketi za kuingia kwenye tukio hilo zikiwa zimeshaanza kuuzwa.
Zaza ni mmoja kati waimbaji ambao wanashikilia kundi zima la Spirit of Praise toka lilipoanza kazi yake akishirikiana na mchungaji Benjamin Dube ambao kwa pamoja wamekuwa wakionekana katika matoleo ya kundi hilo kila mwaka huku pia wakiwa wanawashirikisha waimbaji wengine maarufu wa nchini humo, kama ilivyokuwa kwa mwanaakaka mtume Kekeletso Phoofolo au mwite Keke, Solly Mahlangu, Kgotso Makgalema na wengineo ambapo kwa mwaka huu kwa mara nyingine tena kundi hilo litakuwa na waimbaji walioimba album iliyopita Omega pamoja na Tshepiso huku likiwashirikisha waimbaji kama The Dube brothers, Sello Malete 



« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment