Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, June 21, 2014

Wacheza kamari ya Kombe, wachezwa

Macau, mji ambao biashara yake kubwa ni uchezaji wa kamari 
Polisi wa Macau wanasema wamegundua magengi mawili ya kamari ambayo yamepokea mamilioni ya dola katika kamari ya kubahatisha matokeo ya mechi za Kombe la Dunia.
Maafisa wa polisi wamewakamata watu zaidi ya 20 kwenye hoteli katika mji huo wa kamari.
Watu hao wamekuwa wakipokea simu kutoka sehemu mbalimbali za dunia, na mcheza kamari mmoja amebahatisha zaidi ya dola milioni-5.
Mwandishi wa BBC mjini Hong Kong, jirani na Macau, anasema magengi hayo yakipata dola mia-moja-milioni kila siku kwa wateja wanaobahatisha matokeo ya Kombe la Dunia, na wateja wakiwasiliana nao kwa simu na kwenye internet.
Kati ya watu waliokamatwa 9 ni kutoka Malaysia, 4 kutoka Hong Kong na 13 kutoka Uchina bara.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment