Writen by
sadataley
6:31 PM
-
0
Comments
Na Mussa Juma, MwananchiArusha. Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini, Kanda ya Kaskazini wamethibitisha uwepo wa hazina ya madini ya dhahabu katika Mlima Rankiroga na Mto Karabaline katika Kijiji cha Mgongo, Kata ya Samunge, Wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha.
Kamishna wa Madini Kanda ya Kaskazini, Alex
Magayane alisema jana kuwa Ofisi yake imefanya utafiti wa awali katika
Kijiji cha Mgongo na kubaini uwepo wa dhahabu hiyo.
Wamiminika
Gazeti hili lilikuwa la kwanza kuripoti uwepo wa
dhahabu hiyo baada ya maelfu ya watu kumiminika tena katika eneo la
Samunge, lililokuwa maarufu baada ya Mchungaji Ambilikile Mwasapile
kutangaza kuwa na dawa inayonywewa kwa kikombe kutibu maradhi sugu.
Habari kutoka Samunge zinasema wachimbaji wanazidi
kumiminika kusaka madini hayo yaliyogundulika kuwapo kwenye mashamba ya
watu na maeneo ya kingo za mto huko Mgongo, kijiji kilichopo jirani na
kwa Mchungaji Mwasapile, maarufu kama Babu wa Loliondo.
Diwani wa Samunge, Jackson Sandea alisema maelfu
ya watu kutoka maeneo mbalimbali nchini wamefurika katika kijiji
hicho... “Hadi sasa kuna watu zaidi ya 4,000 na bado wanaongezeka. Hii
inaweza kuwa ni zaidi ya kipindi kile cha Babu. Dhahabu hii inapatikana
mtoni tu. Watu wanakusanya michanga na kupata dhahabu, hakuna mtu ambaye
anachimba.”
Alisema tofauti na maeneo mengine, dhahabu ya
Samunge inaonekana ni ya Watanzania wote kwani ipo eneo la mto ambao
unamilikiwa na Serikali na ndiyo sababu watu wanaingia kwa wingi. “Kuna
wengine wanapata (dhahabu), hata mashambani lakini mtoni ndipo
inapatikana kwa wingi zaidi.”
Matokeo ya utafiti
“Ni kweli kuna dhahabu katika eneo la Mto
Karabaline na kiasi kikubwa kipo katika eneo la Mlima Rankiroga,”
alisema Magayane. Mlima huo upo jirani na Mto Karabaline ambako dhahabu
ilianza kugundulika. Wachimbaji wamekuwa wakiomba idhini ya Serikali
kuchimba dhahabu katika mlima huo.
Magayane aliwataja wataalamu waliofanya utafiti
huo kuwa ni Mtaalamu wa Miamba, Fatuma Kijanda; Fundi Sanifu Mkuu,
Zephelin Kalunde na Fundi Sanifu Mwandamizi, Aloyce Mlaga.
Alisema uchunguzi zaidi unaendelea ili kujua ujazo
wa dhahabu katika eneo hilo na muda ambao uchimbaji unaweza kuchukua...
“Tumepeleka baadhi ya miamba katika ofisi za uchunguzi Dodoma na
tunatarajia kupata taarifa karibuni.”
Hata hivyo, alisema dhahabu inayopatikana kwenye
Mto Karabaline inaweza kumalizika ndani ya miaka miwili tofauti na ile
ya mlimani ambayo alidokeza kuwa itachukua muda kuisha.
Ingia hapa https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=1326918772453457809#editor/target=post;postID=3015600058097478983
Ingia hapa https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=1326918772453457809#editor/target=post;postID=3015600058097478983
No comments
Post a Comment