Writen by
sadataley
5:36 PM
-
0
Comments
Mshambuliaji wa Ufaransa, Karim Benzema (katikati) akipiga shuti ambalo
liligonga mwamba na kipa wa Honduras, Luis Lopez (kushoto) akajifunga
wakati akijaribu kuzuia shuti hilo hivyo kuipatia Ufaransa bao la pili
katika mechi ya kundi E ya Fainali za Kombe la Dunia kwenye Uwanja wa
Beira-Rio mjini Porto Alegre jana. Ufaransa ilishinda 3-0. Picha na AFP.
Porto Alegre, Brazil. Ufaransa imeanza vyema Fainali za Kombe la Dunia baada ya kuichapa Honduras mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Beira-Rio mjini Porto Alegre, Brazil na kuongoza kundi E.
Katika dakika ya 43, Ufaransa ilipata penalti
baada ya Wilson Palacios kumsukuma Paul Pogba kwenye eneo la hatari na
mwamuzi kumpa kadi ya pili ya njano Palacios na kadi nyekundu.
Mshambuliaji Karim Benzema alipiga penalti hiyo na
kuipatia Ufaransa bao la kwanza kabla ya dakika ya 48 kipa Noel
Valladares kujifunga akijaribu kuzuia shuti la Benzema na hivyo Ufaransa
kupata bao la pili.
Kama hiyo haitoshi, dakika ya 72, Benzema
aliipatia Ufaransa bao la tatu kwa shuti kali baada ya shuti la Mathieu
Debuchy kuzuiliwa. Hivi sasa Ufaransa inaongoza kundi E ikifuatiwa na
Uswisi, Ecuador na Honduras.
Katika mechi ya awali, Uswisi iliibuka na ushindi
wa mabao 2-1 dhidi ya Ecuador katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa
Nacional Mane Garrincha mjini Brasilia. Mechi hiyo ambayo ilihudhuriwa
na mashabiki 68,351, Ecuador ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao katika
dakika ya 22 lililofungwa na Enner Valencia kwa kichwa akiunganisha
mpira wa faulo uliopigwa na Walter Ayovi, lakini Uswisi walisawazisha
bao hilo katika dakika ya 48 mfungaji akiwa Admir Mehmedi kwa kichwa
akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Ricardo Rodriguez.
Mechi ikiwa inaonekana itamalizika kwa sare, Haris
Seferovic akiwa ametokea benchi aliipatia Uswisi bao la pili katika
dakika ya 90+3 akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Rodriguez.
No comments
Post a Comment