Writen by
sadataley
12:02 PM
-
0
Comments

Kundi la Boko Haram limekiri kuwateka nyara wasichana hao na kusema kuwa litawauza
Polisi nchini Nigeria wameahidi kumtunuku dola laki
tatu za marekani yeyote atakayetoa habari zitakazowasaidia kuwapata
zaidi ya wasichana mia mbili waliotekwa na kundi la wapiganaji wa boko
haram mwezi uliopita .
Juma lililopita Wapiganaji wa Boko Haram
walisema kuwa wasichana hao 200 kutoka eneo la Chibok waliotekwa mwezi
uliopita watauzwa.Aidha Maafisa nchini Nigeria Wamesema kuwa idadi ya wasichana zaidi waliotekwa nyara na kundi la wapiganaji wa kiislamu wa Boko Haram imetimu 11.
8 kati yao walitekwa kutoka kijiji cha Warabe kilichoko katika jimbo la Borno siku ya jumapili nao watatu zaidi wakatekwa kutoka kijiji jirani .
Rais wa Marekani ameingilia swala hilo akisema kuwa serikali yake itatoa msaada ili kuwakomesha wapiganaji hao.
Tayari marekani imewatuma maafisa kadhaa kusaidia kusuluhisha kwa amani kitendawili cha utekaji nyara huo.
No comments
Post a Comment