Writen by
sadataley
12:03 PM
-
0
Comments

Juhudi za serikali dhidi ya kundi hilo hazijaonekana kuzaa matunda
Taarifa kutoka nchini Nigeria, zinasema kuwa mamia ya
watu waliuawa katika shambulizi lililofanywa na kundi la wapiganaji wa
Boko Haram katika mpaka wa nchi hiyo na Cameroon siku ya Jumanne.
Katika mahojiano na BBC kiongozi mmoja wa eneo
hilo, Ahmed Zanna, alisema kuwa washukiwa walivamia mji wa Gamboru
Ngala, katika jimbo la Borno, na kuwaua takriban watu 300.Inaarifiwa wapiganaji hao waliwafyatulia risasi watu kiholela katika soko kuu la eneo hilo.
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria anasema ilikuwa vigumu kupata taarifa hizo mapema kwa sababu ya changamoto ya mawasiliano katika jimbo hilo hasa kwa sababu eneo hilo liko mbali sana.
Wakazi wa eneo hilo wanasema kuwa walipata zaidi ya maiti miamoja kutokana na shambulizi hilo.
No comments
Post a Comment