Writen by
sadataley
10:37 AM
-
0
Comments
Mawaziri wengine wamekuwa wakiwekwa kitimoto
kutokana na tuhuma za utendaji mbovu na udhaifu kwenye wizara zao,
lakini hali ilikuwa tofauti jana wakati Waziri Kivuli wa Ardhi, Halima
Mdee aliposoma hotuba ya kurasa 77 ya upinzani kuhusu makadirio na
matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, huku kurasa
30 zikielekeza tuhuma kwa waziri huyo.
Miongoni mwa tuhuma zilizotolewa dhidi ya waziri
huyo ni pamoja na kujinufaisha kupitia mgogoro wa ardhi katika eneo la
Chasimba na kiwanda cha Saruji cha Wazo Hill jijini Dar es Salaam.
Mdee, ambaye pia ni mbunge wa Kawe, alimhusisha
waziri huyo na ufisadi katika kazi ya utafiti uliofanywa na wataalamu wa
masuala ya ardhi, uliogharimu Sh700 milioni. Tuhuma hizo zilimchanganya
Waziri Tibaijuka kiasi kwamba wakati akitoa majibu alijikuta akitoka
nje ya mada na kumshambulia Mdee, huku Spika Anne Makinda akimrudisha
kila mara na kumtaka ajikite kwenye hoja na kuacha kushambulia
wapinzani.
Waziri Tibaijuka pia alidai hotuba ya upinzani ilijaa uongo na kumtaka Spika Makinda kumchukulia hatua Mdee.
Akisoma maoni ya Kambi ya Upinzani bungeni jana,
Mdee alisema utafiti huo ulikuwa na timu ya watu 140 kutoka taasisi
mbalimbali ikiwemo, sekta binafsi na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM).
Alisema waziri huyo anatuhumiwa kuingilia mchakato
huo kwa kuingiza jamaa zake na taasisi ambazo ana uhusiano nazo kama
sehemu ya kikosi kazi cha utafiti kwa jina la wataalamu washauri.
“Matokeo yake, Idara ya Uchumi ya UDSM ilitumika
kama chambo huku kiasi kikubwa kikimrudia mwenyewe kwa mlango wa nyuma,”
alisema Mdee.
“Ilifika hatua wataalamu walimsusia kazi waziri
kutokana na kuwepo ujanja ujanja katika masuala ya fedha, hivyo
kumlazimu waziri kujifungia na wasaidizi wake kukamilisha kazi
iliyobaki.”
Kadhalika Mdee alimtuhumu Tibaijuka kwamba ana
uhusiano na Taasisi ya Tanzania Women Land Access Trust (TAWLAT) ambayo
ililipwa kiasi cha Sh300 milioni kutoka Manispaa ya Kinondoni kwa ajili
ya kutoa elimu na kuendesha mazungumzo kwa diplomasia, kati ya viongozi
na wananchi wa Chasimba kuhusu mgogoro wa ardhi.
“Licha ya kulipwa fedha hizo, TAWLAT haikufanya
kazi yoyote ya uthamini katika eneo la Chasimba, badala yake aliyekuwa
mkurugenzi wa upimaji, mthamini mkuu wa serikali pamoja na wataalamu wa
wizara walikuja kuniomba niwatulize wananchi waliokuwa wanawarushia mawe
kwa kuwa hawakuwa na imani na viongozi hao,” alisema Mdee.
Mdee, ambaye pia ni mbunge wa Kawe (Chadema),
aliitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru),
kuichunguza TAWLAT kuhusu ushiriki wake aliosema una shaka katika kazi
kadhaa za Wizara ya Ardhi.
Kwa habari zaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Mdee-amvuruga-Tibaijuka/-/1597296/2329902/-/52j5exz/-/index.html
Kwa habari zaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Mdee-amvuruga-Tibaijuka/-/1597296/2329902/-/52j5exz/-/index.html
No comments
Post a Comment