Writen by
sadataley
10:35 AM
-
0
Comments
Hatimaye tume ya uchaguzi nchini Malawi imesema itatangaza matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kesho ijumaa.
Uamuzi huo unakuja baada ya mivutano na mapingamizi kadhaa kwenye mahakama kuu nchini humo.Taarifa fupi iliyotolewa na tume ya uchaguzi jana usiku mjini Blantyre, imesema wameamua kutangaza matokeo hayo kwa kuzingatia sheria inayoibana kufanya hivyo ndani ya siku zisizozidi nane na ikiwa ni baada ya saa 48 tangu kumaliza hesabu ya kura.
Kwa siku mbili sasa kumekuwa na tuhuma za kuokotwa kwa baadhi ya masanduku ya kura, huku baadhi ya magari ya yakipatikana na masanduku ya kura na hata katika baadhi ya maeneo ambako ilielezwa kuwa kura zimehifadhiwa, usalama wake umesemwa kuwa mdogo.
Mmoja kati ya wananchi wa nchi hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Malani Nyirenda, alielezea hisia zake alipozungumza na BBC mjini Lilongwe kutokana na suala la kuchelewa kutolewa matokeo na mpango wa kuhesabu upya kura za baadhi ya maeneo.
Tume hiyo imesema hadi kufikia sasa imepokea malalamiko 275 na imekwisha yafanyia kazi malalamiko 170 tu.
No comments
Post a Comment