Writen by
sadataley
9:37 AM
-
0
Comments
Dodoma. Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kwa siku ya pili jana alikuwa katika wakati mgumu kuunda baraza jipya kivuli la mawaziri.
Baraza hilo ambalo kwa mara ya kwanza litajumuisha
wabunge kutoka vyama vya vingine vya upinzani vya NCCR-Mageuzi na CUF
lilikuwa litangazwe jana. Baraza Kivuli lililokuwapo lilijumuisha
wabunge wa Chadema pekee.
Habari za uhakika zilizopatikana jana zilisema
kuwa juzi Mbowe na wasaidizi wake wa karibu alikuwa akiunda baraza lake
hilo hadi saa 8:00 usiku wa kuamkia.
“Yuko kwenye hatua za mwisho kukamilisha Baraza
hilo … jana (juzi) amefanya kazi hiyo hadi saa 8:00 usiku wa manane,”
kilidokeza chanzo kimoja.
Baraza hilo jipya linaonekana kuvuta hisia za
wabunge wengi wa CCM kutokana na baadhi yao kuligusia wakati wakichangia
Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Miongoni mwa wanaotajwa kuingizwa katika baraza
hilo ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, Mbunge wa Kigoma
Kusini, David Kafulila na Mbunge wa Mkanyageni kupitia CUF, Mohamed
Habib Mnyaa.
Kuingizwa katika Baraza hilo kivuli kwa wabunge wa
NCCR-Mageuzi na CUF ni matunda ya ushirikiano wa Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) ulioasisiwa wakati wa Bunge Maalumu la Katiba.
Umoja huo ndio uliowaongoza wajumbe karibu 200 wa Bunge Maalumu la Katiba kususia vikao vya Bunge Maalumu la Katiba.
Alipoulizwa kuhusu ahadi yake ya kutangaza baraza hilo jana, Mbowe alisema ameahirisha na sasa atalitangaza leo.
“Nafahamu wabunge na wananchi wana shauku ya
kufahamu watakaoingia katika baraza kivuli lakini naomba niseme
sitalitangaza leo kama nilivyoahidi,” alisema.
No comments
Post a Comment