Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, April 1, 2014

Matunda na Mboga zinaokoa maisha

Mboga za majani ndizo nzuri zaidi katika afya ya mtu
Watafiti nchini Uingereza wanasema kula matunda na mboga za majani mara saba kwa siku inakuwezesha kuwa na afya zaidi kuliko mara tano iliyokuwa imependekezwa hapo awali na shirika la afya duniani
Utafiti huu mpya unasema kuwa kula matunda mara saba kwa siku kunaweza kuokoa maisha yako kutokana na vifo vya mapema.
Eti wanasema kuwa ikiwa utakula matunda mara saba kwa wiki uwezo wako wa kupatwa na magonjwa yanayotishia maisha yako, unapungua kwa asilimia 42.Utafiti uliofanyiwa wanaume na wanawake, 65,226, ulionyesha kuwa matunda mengi aliyokula mtu mmoja yalimpunguzia uwezo wa kufariki katika umri wowote.
Wataalamu wanasema kuwa mifumo mingine ya maisha kama vile kutovuta sigara na kutokunywa pombe kupindukia pia imechangia kupungua kwa vifo.
Wanasema kuwa hawakuzingatia tu faida za Matunda na mboga bali mambo mengine mengi.

Watafiti katika Chuo kikuu cha University College London, walitathmini Data iliyokusanywa kati ya mwaka 2001 na 2008, iliyowapa mweleko kuhusu afya ya watu wanaokula matunda kwa wingi.
Utafiti huo ulitathmini idadi ya vifo kwa ujumla pamoja na vifo vinavyotokana na Saratani, maradhi ya Moyo na Kiharusi na kugundua kuwa vifo vya mapema vilipungua kulingana na mtu anavyokula matunda na mboga za majani.
Mboga za majani ndizo zilikuwa na uwezo mkubwa wa kulinda mwili dhidi ya maradhi hjata zaidi ya matunda.
Maji ya matunda hayakuwa na manufaa makubwa huku matunda yanayopakiwa kwenye mikebe yakionekana kuongeza tisho la kifo.

Wataalamu wanasema kuwa wangali wanaendelea na utafiti wao na kwamba kuna mambo mengine mengi yanayochangia afya ya mtu.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment