Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, February 20, 2014

Rais wa Ukraine asema kuna mwafaka

Waandamanaji nchini Ukraine
Rais wa Ukraine, Viktor Yanukovych, na viongozi wa upinzani wamefikia makubaliano katika jitihada za kusitisha ghasia kali za hivi maajuzi kati ya polisi na waandamanaji wanaoipinga serikali katika mji mkuu Kiev na kwengineko.
Kufuatia mazungumzo na viongozi watatu wakuu wa upinzani, rais Yanukovych alitoa taarifa rasmi iliyosema kwamba walikubaliana kujadiliana yalionuiwa kusitisha umwagikaji damu. Viongozi wawili wa upinzani Vitali Klitschko na Arseniy Yatsenyuk, wamesema rais huyo alitoa hakikisho kwamba kambi za waandamanji katikati mwa mji wa Kiev hazitovamiwa.
"Duru ya kwanza ya mazungumzo imekamilishwa na nina furaha kwa sababu tunachukuwa hatua ya kusitisha vurugu na nina matumaini kwamba leo usiku hatutakuwa tukipigana tena kwa sababu kesho asubuhi tutaketi tena kutafuta mwafaka kati ya upinzani na serikali," amesema Vitali KlitshkoVitaliy Klitschko, ameiambia BBC amefurahishwa na hatua iliyopigwa mpaka sasa.

Moto unaendelea kuwaka katika bustani ya Independence Square huku waandamanji na polisi ya kupambana na fujo wakiwa katika mkwamo.Naibu waziri mkuu wa Ukraine, Konsti-antyn Gry-shchenko ameiambia BBC kwamba upinzani unahitaji kudhibiti alichokitaja kuwa kundi la wafuasi wadogo ambalo anasema ndilo lililosababisha ghasia hizo.
Ghasia nchini Ukraine
"Tatizo tunalokabiliana nalo sio upinzani wa kiasa, sana sana linatokana na nguvu za watu wenye misimamo mikali ambao hawasikii upinzani. Wanabuni tatizo kubwa kwa kutumia vurugu na kasoro yao ya kutosikizana. Tunahitaji kupata suluhu ambapo wale wanaowajibika kisiasa watahakikisha kwamba kwamba watu hawa wachache wanaosababisha vurugu wanaulizwa maswali na kuthibitiwa."

Watu wapatao 26 wameuawa na mamia wengine wamejeruhiwa tangu kuzuka ghasia hizo siku ya Jumanne.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment