Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, February 20, 2014

Jamaa za Korea kuunganishwa tena leo

Hawajaonana kwa kipindi cha miaka 60.
Makundi kadhaa ya watu wakongwe kutoka Korea Kusini wanaelekea Kaskazini kukutana na jamaa zao ambao hawajaonana kwa zaidi ya miaka sitini, tangu vita vilivyotenganisha mataifa hayo mawili ya rasi ya Korea.
Wakongwe hao wamebeba mikoba iliyojaa zawadi, ikiwa ni pamoja na dawa za maradhi ya kawaida, picha za familia na vyakula.
Tukio hilo litakaloibua majonzi litafanyika katika eneo la kitalii upande wa Korea Kaskazini.
Hapajakuwa na zoezi kama hilo la kuunganisha familia tangu mwaka 2010.
Awali Korea Kaskazini imefutilia mbali mpango huo wa kuziunganisha familia kujibu vitendo vya Korea Kusini ambavyo Kaskazini inapinga.
Shirika la Msalaba Mwekundu linasema kuwa watu alfu sabini wanaoishi Kusini wanasubiri fursa ya kukutana na jamaa zao wa Kaskazini-nusu kati ya watu hao ni wazee walio na umri wa zaidi ya miaka 80.
Chanzo:bbc swahili
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment