Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, January 28, 2014

JASUSI WA AL-SHABAAB AUAWA SOMALIA.

somali_25598.jpg
Wakaazi wa Kusini mwa Somalia, wameiambia BBC kuwa kamanda mmoja mkuu wa kundi la wanamgambo la Al Shabaab ameuawa katika shambulizi la kombora.
Shambulizi hilo lilifanywa na wanajeshi wa Marekani.
Wamesema kuwa kamanda huyo Sahal Iskudhuq, na wapiganaji wengine wanne wa kundi hilo, wameuawa kwenye shambulizi hilo.
Kombora liligonga gari la wanamgambo hao ambalo walikuwa wanasafiria karibu na mji wa pwani wa Barawe.
 Taarifa hizi hata hivyo bado hazijathibitishwa na jeshi la Marekani.
Iskudhuq inasemekana alikuwa na uhusiano wa karibu sana na kiongozi wa Al Shabaab Ahmed Abdi Godane na kamanda mkuu wa kitengo cha ujasusi cha kundi hilo kijulikanacho kama Amniyat.
Al Shabaab wameondoka kutoka katika miji mikubwa ya Somalia ikiwemo Mogadishu ingawa bado wanadhibiti sehemu kubwa za nchi.
Chanzo ni bbcswahili.com
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment