Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, January 28, 2014

AU YAONDOA VIKWAZO DHIDI YA MADAGASCAR

MADAG_c4d1c.jpg
Umoja wa Afrika umeondoa vikwazo dhidi ya Madagascar na kusema nchi hiyo imekamilisha kipindi chake cha mpito na kurudisha utawala wa kikatiba.
Baraza la Amani na Usalama la AU liliamua Jumatatu kumaliza marufuku hiyo iliyowekwa baada ya mapinduzi ya mwaka 2009 na kuikaribisha Madagascar kurudi mara moja kwenye ushiriki wake.
Rais Hery Rajaonarimpianina alichukua madaraka Jumamosi baada ya kushinda uchaguzi mwezi Desemba.
Umoja wa Afrika ulitaja uchaguzi wa rais na wabunge katika maamuzi yake ya Jumatatu, wakionyesha shukrani kwa watu wa Madagascar kwa hatua iliyojumuisha watu wote, yenye kuaminika na iliyo ya halali.
Chanzo, voaswahili.com
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment