Writen by
sadataley
7:11 AM
-
0
Comments
CHADEMA yamfunga Zitto
SIKU moja baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kukubali pingamizi la Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kuizuia Kamati Kuu (CC) ya CHADEMA isimjadili hadi kesi yake ya msingi itakapokuwa imesikilizwa, chama hicho kimemfungia rasmi kushirikiana na wabunge wenzake katika shughuli za kisiasa.
Sambamba na hilo, chama hicho kimesema kuwa kuanzia sasa kinasahau mjadala kuhusu Mbunge huyo wa Kigoma na badala yake kinajikita kuchapa kazi kwa ajili ya malengo waliyojiwekea mwaka huu 2014.
Shughuli ambazo Zitto amefungiwa nazo ni pamoja na zile za nje na ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano, hususani zinazohusu kambi rasmi ya upinzani bungeni, inayoongozwa na CHADEMA.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano Habari na Uenezi, CHADEMA, John Mnyika, alisema uamuzi wa mahakama haujaelekeza kwamba Zitto apewe ushirikiano na chama chake, hivyo uamuzi wa CC wa kutoshirikiana naye uko pale pale.
Katika uamuzi wa CC uliosomwa na Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, pamoja na kutangaza uamuzi wa kuwavua uanachama Samson Mwigamba na Dk. Kitila Mkumbo, alisema: “Kwa vile Zitto Zuberi Kabwe amekishitaki chama kinyume na matakwa ya katiba ya chama na kanuni zake, na kwa vile Mahakama Kuu imeamuru vikao vyote vya chama visijadili wala kuamua suala lolote linalohusu uanachama wa Zitto, viongozi wa ngazi zote za chama wanachama, washabiki na wapenzi wa CHADEMA popote walipo katika nchi yetu na nje ya Tanzania, wasishiriki wala kusaidia kwa namna yoyote mikutano yoyote ya nje au ndani au shughuli nyingine yoyote ya kisiasa itakayofanywa na Zitto na mawakala wake kwa jina la CHADEMA.”

Mnyika alisema Kamati Kuu ilishapitisha azimio la kumtenga Zitto na shughuli za siasa na kuwataka wanachama wao kote nchini, wasitoe ushirikiano kwa kazi au shughuli yoyote itakayofanywa na mbunge huyo.
“Uamuzi huo upo pale pale, na mahakama haijaelekeza kwamba apewe ushirikiano,” alisema Mnyika wakati akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu.
Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo, aliwataka wafuasi wa CHADEMA kutambua kuwa kilichoamriwa na mahakama ni pingamizi la awali tu kwani kesi ya msingi bado haijaanza kusikilizwa.
“Unajua kilichoamriwa ni pingamizi la awali. Huko ni sawa na kushangilia bao wakati mpira ndio kwanza umeanza na unaendelea. Mfano mzuri ni kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Simba na Yanga. Yanga walishangilia mabao matatu ya kipindi cha kwanza wakijua wameshinda, walipoingia kipindi cha pili unajua kilichotokea… Kwa hiyo kesi ya msingi bado, na hatuoni sababu ya kushangilia kwa sasa,” alisema.
No comments
Post a Comment