Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, October 4, 2013

KWA TAARIFA YAKO: NYOTA WA FILAMU NIGERIA ALIYEACHANA NA FILAMU NA KUWA MUHUBIRI

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu

Lizy na mumewe askofu Great Emeya.
KWA TAARIFA YAKO je unajua kuhusu mwigizaji nyota wa filamu Nigeria aitwaye Elizabeth Benson ama Lizy kama wapenzi wake wapendavyo kumuita alikacha uigzaji mnamo mwaka 1996 baada ya kuokoka?, mwanamama huyu mwenye mvuto wa kipekee na aliyejaliwa kipaji cha hali ya juu katika ugizaji, aliacha kuigiza wakati ambao jina lake lilikuwa midomoni mwa wananchi wengi wa nchini kwake Nigeria na nje ya nchi hiyo ambao walimpenda kutokana na uigizaji wake.
Moja ya filamu aliyoigiza vyema kwakushirikiana na mwanamama Hilda Dokubo.
Kutokana na kuokoka huko, mwanamama huyo ambaye kati ya filamu zake zilizompatia umaarufu ni pamoja na "Hour of Grace" aliyoigiza kama mke mwenza wa mwanamama mwingine nyota Hilda Dokubo, aliamua kujikita katika kuhubiri injili ya Mungu wetu. KWA TAARIFA YAKO kama hilo halitoshi mwanamama huyo alifanya jambo la kustukiza na kuwaacha watu midomo wazi baada ya kufunga ndoa mwaka 2009 na askofu Great Emeya ambaye anatunza kanisa la Rainbow Christian Assembly huko jimbo la Delta huku mkewe yaani Eliza akitumia nafasi yake ya uinjilisti kumtangaza Kristo. Ndoa ya mwigizaji huyu ilikuja kufuatia kukaa maisha ya ujane kwa muda mrefu baada ya mumewe wa kwanza Samuel Gabriel Etim kufariki dunia wakati mwanamama huyo akiwa katika umri wa miaka ya 20 akiachiwa kulea watoto ambao anamshukuru Mungu wamekua kwasasa.
Lizy siku ya harusi yake mwaka 2009

KWA TAARIFA YAKO baada ya kupotea kwa kipindi kirefu na kurejea tena miaka ya 2000 katika ugizaji, mwanamama huyo amefurahi kwakuwa mumewe amemruhusu kuendelea na kazi yake ya uigazi ambayo Lizy mwenyewe amesema anaitumia katika kumrudishia na kuutangaza ukuu wa Mungu. Lizy ana watoto watatu ambao alipata na marehemu mumewe ambapo wawili kati ya hao watoto wake wanakaa nchini Uingereza na mmoja yupo Nigeria huku akisema kwamba anamshukuru Mungu ameolewa na mjane mwenzake ambaye ni mtumishi wa Mungu anayechunga kanisa kubwa sana huko Warri hali ambayo itamfanya huduma yake ya Uinjilisti kusonga mbele.
Habari kwa hisani ya http://gospelkitaa.blogspot.com
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment