Writen by
sadataley
5:22 PM
-
0
Comments
Takribani watu 51 wameuawa na wengine zaidi ya mia moja kujeruhiwa kufuatia shambulizi lililolenga washia huko mji mkuu wa Iraq Baghdad,wizara ya mambo ya ndani imethibitisha.
Moja kati ya shambulizi la hivi karibuni mjini Baghdad nchini Iraq
REUTERS/StringerKatika mji wa Balad shambulizi la kujitoa muhanga limeua takribani watu 12 katika mgahawa wakati na huko Masul watu wenye silaha wameshambulia na kuua waandishi wa habari wawili.
Iraq imeendelea kushuhudia vita vya kidini katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni matukio ambayo yameyumbisha hali ya usalama nchini humo.
Hata hivyo hakuna kundi lililojitokeza kudai kuhusika na shambulizi hilo la jumamosi ingawa matukio mengi ya hivi karibuni yamekuwa yakitekelezwa na mashirika ya kisuni yenye uhusiano na kundi la kigaidi la Al Qaeada.
No comments
Post a Comment