Writen by
sadataley
10:24 AM
-
0
Comments
Polisi nchini Nigeria wanawasaka wanaume waliomteka nyara kiongozi wa ngazi ya pili wa kanisa la kianglikana nchini Nigeria Askofu mkuu Ignatius Kattey.
Askofu Ignatius Kattey
Askofu Ignatius ni mkuu wa kanisa la kianglikana tawi la jimbo la Niger Delta.
Katika miaka ya hivi karibuni, visa vya watu kuteka nyara wakati wakidai kulipwa kikombozi vimekuwa jambo la kawaida katika jimbo lenye utajiri wa mafuta la Niger Delta linalozingira Port HarcourtAlitekwa nyara Ijumaa jioni akiwa na mkewe Beatrice, karibu na makao yao mjini Port Harcourt, Kusini mwa nchi.
Mwaka jana mamake waziri wa fedha, Ngozi Okonjo-Iweala alitekwa nyara na kuzuiliwa kwa siku tano.
Hakuna kundi lolote limedai kumkamta Askofu huyo akiwa na mkewe.
Makundi mengi ya magenge ya watu waliojihami, huendesha shughuli zao katika eneo hilo kutokana na miaka mingi ya migogoro katika eneo hilo dhidi ya sekta ya mafuta.
No comments
Post a Comment