Writen by
sadataley
11:06 AM
-
0
Comments

“Tunawezesha wanawake maeneo mengi duniani; Afrika, Amerika ya Kati, Marekani, Ulaya na kwingineko duniani na zaidi ni kuwasaidia wanawake, ambao nao hutoa mafunzo.”
Na Mwandishi Wetu, Mwananchi
Mpango huo unalenga kusaidia wanawake, baada ya kuhitimu watawafundisha wenzao
Morogoro. Shirika la Oxfam Tanzania limesema mpango uliopo hivi sasa ni kuwezesha wanawake zaidi kiuchumi, likiamini wakiwezesha wanakuwa wazalishaji wazuri
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam, Jane Foster, alipotembelea shamba darasa lililowezeshwa kwa Sista Martha Mwasu, mkoani Morogoro.
Foster alisema maendeleo ya wanawake yanaonekana kupitia mpango wa shirika lake, ambalo tangu mwaka 2011 limewakomboa zaidi ya Watanzania milioni 25.
“Tunawawezesha wanawake maeneo mengi duniani; Afrika, Amerika ya Kati, Marekani, Ulaya na kwingineko duniani na zaidi ni kuwasaidia wanawake, ambao na wao hutoa mafunzo iwe kwa wanawake au wanaume kupitia mtu mmojammoja au vikundi,” alisema.
Naye Mkuu wa Wilaya Mvomero, Anthony Mtaka, aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa shamba darasa, alisema: “Napongeza mpango huu kuwasaidiwa wanawake, haya ndiyo maisha ya kila siku ambayo leo hii watu wakiungana wakawezeshwa, taifa litaneemeka.” Pia, alipongeza Oxfam na mashirika hisani, kusaidia wanawake kwani wao ndiyo wazalishaji wakubwa na ndiyo wanaolisha taifa.
Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja Kampeni, Ushawishi na Utetezi, Mwanahamisi Salim, alisema ujenzi wa mradi huo ambao kwa sasa una vijana 12, umegharimu zaidi ya Sh10 milioni.
Hata hivyo, Salim alisema changamoto inayolikumba shamba hilo, ni ukosefu wa maji ambayo ni ya mgawo lakini mpango uliopo ni kuchimba visima vya kisasa kusaidia umwagiliaji.
Alisema mpango huo ukikamilisha utasaidia kumaliza tatizo hilo, ambao linakwamisha maendeleo ya shamba hilo.
Chanzo:www.mwananchi.co.tz
No comments
Post a Comment